... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hekima Inayowawia Vigumu Watu Kuikubali

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 2:7,8 Bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambaye wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu.

Listen to the radio broadcast of

Hekima Inayowawia Vigumu Watu Kuikubali


Download audio file

Wenye mamlaka na madaraka duniani – yaani watawala wa mataifa, mabiliyonea, mashuhuri, “washawishi” mtandaoni – wote wanafanana kwa mambo mawili.  Kwa muda huu, kweli wana ushawishi mkubwa mno, lakini siku moja, wote watatoweka.

Je!  Umewahi kutafakari ni yapi yanayoshawishi mawazo yako?  Ni yapi yanayotengeneza maoni yako hata mwitikio wako kuhusu yanayopitika katika jamii siku hizi, pia yanayotokea maishani mwako?

Vinavyojulikana kuwa hekima, vimebadilika sana hii miaka hamsini iliyopita.  Maadili ya kale yametupwa nje na watu wamepokea mfumo wa uadilifu usio na msingi wo wote.  Jamii imevurugika, imepoteza umoja na ushirikiano na mgogoro huu umesukumwa na kelele za watu wachache ambao wana ushawishi mkubwa.

Katikati ya fujo iliyopo, Yesu anatujia na hekima ambayo tunafahamu kwenye kiini cha mioyo yetu kwamba inafanya kazi kweli kweli – lakini kwa watu wengi, ni hekima inayowawia vigumu kuikubali.  Tumsikilize tena Mtume Paulo akiwaandika Wakorintho miaka elfu mbili iliyopita:

1 Wakorintho 2:7,8  Bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu.

Zamani, hekima ya Mungu iliwakwaza watu mno, kiasi cha kuwafanya wamgongomee Yesu msalabani kwa sababu aliitetea.  Wenye mamlaka na wafuasi wao daima wamekataa na kupinga hekima ya Mungu, si jambo jipya hata kidogo, na wataendelea kuikataa.  Kama kweli wangaliijua wasingemtundika msalabani.  

Na Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.