... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Jaribu la Tatu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 4:8-11 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia. Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.

Listen to the radio broadcast of

Jaribu la Tatu


Download audio file

Ni yapi humu ulimwenguni unayatamani sana?  Ni anasa gani?  Mali gani?  Ni kitu gani unatamani kupata hapa duniani?  Halafu niulize pia, Je! Uko tayari kugharimia nini ili ukipate?

Ni jambo la kawaida kabisa mtu kuwa na matumaini na shauku kupata mali na anasa kama nilivyosema.  Ni kawaida, apende kujulikana, kuheshimiwa na kuwa na cheo na mamlaka.  Mambo hayo yanatuvuta polepole yakitushawishi chinichini mpaka pale yanapotunasa tusipoweza tena kupinga.

Lakini kadiri mtu anavyozidi kupenda vitu vya ulimwengu huu, ndivyo anavyozidi kupelekwa mbali na makusudi ya Mungu kwa ajili ya maisha yake.  Huwezi kufuata vyote viwili.

Mathayo 4:8-11  Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.  Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.  Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.

Shetani alimjaribu Yesu pale alipokuwa mnyonge kwasababu ya kukosa chakula baada ya kufunga siku arobaini nyikani. mtu anajitahidi kumtumikia Mungu lakini ikionekana kama matokeo yake ni mateso makubwa, mapambo ya dunia yenye yatazidi kuwa na vivutio vyenye nguvu.  Shetani anajua hayo.  Kwahiyo, akikujia katika mazingira magumu na kukuvuta na jaribu kama hilo, kumbuka maneno haya:  Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy