... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kitu Ambacho Mungu Hawezi Kukibariki

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Isaya 59:1,2 Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.

Listen to the radio broadcast of

Kitu Ambacho Mungu Hawezi Kukibariki


Download audio file

Kuna wakati inaonekana kama Mungu yuko mbali nasi kiasi cha kilomita milioni naa.  Hisia kama hizo zinatatanisha sana, unahisi kama kuna pengo

Labda leo unatazamia nikwambie habari za baraka za Mungu na hatima nzuri Mungu alizoandaa kwa ajili yako na mema yote anayotaka kukukirimia.  Hata kama hayo ni kweli na sahihi, leo sitaleta ujumbe kama huo.

Mzizi unaosababisha tutengane na Mungu, ni pale  sisi tunapoamua kufuata njia zetu wenyewe. Mtu anaweza kusema, Ndiyo, Neno la Mungu linasema hili jambo ni kosa na halimletei Mungu utukufu … lakini hayo yalitamkwa miaka maelfu iliyopita. Mimi ninafahamu vizuri.

Hivyo hivyo, kidogo-kidogo mambo yanakuharibikia; halafu ghafla, maisha yanakumwagia matatizo makubwa kichwani mwako na Mungu anaonekana kuwa mbali nawe kiasi cha kilomita milioni. Sasa yafuatayo yanaelezea kinachoendelea hapo:

Isaya 59:1,2  Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.

Nineno lisilopingika:  Mungu hawezi kubariki yale aliyokataza mwenyewe.

Kwa kuwa anakupenda, hawezi kabisa kubembeleza au kubariki au kupuuza dhambi yako.  Ila, kupitia Yesu, anaweza kukusamehe ukiacha ile dhambi na kumrudia yeye.  Mara moja atakuwa karibu yako kuliko siri iliyofichwa kwenye kiini cha moyo wako, kwa sababu …

Uwezo wa Bwana bado unatosha kukuokoa.  Atakusikia wakati unamwomba akusaidie.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.