Kukaa Bila Kuoa au Kuolewa (1)
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
1 Wakorintho 7:8,9 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.
Hata kama watu karibu wote wanafunga ndoa, si wote wanaendelea kudumu kwenye ndoa zao. Kinachonihuzunisha ni kwamba, wengine wanawaangalia na kujiuliza kama wana tatizo au upungufu fulani.
Mimi binafsi sikuitwa ili niishi bila kuoa. Nafurahi sana kwamba nina uhusiano mzuri tena wa karibu sana na mke wangu mrembo. Lakini hali hiyo si kwa kila mtu:
1 Wakorintho 7:8,9 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.
Kwanini Mtume Paulo anasema kwamba ni heri kutokuoa au kuolewa? Kesho ndipo tutachunguza jibu la swali hilo na tutagundua kwamba kubaki bila kuoa ni wito wa hali ya juu.
Kama hujisikii una haja ya kuoa au kuolewa acha tu. Usibanwe na mawazo au matazamio ya watu wengine na kuingia katika vifungo vya kuishi na mtu ambaye hakukusudiwa kuwa mwenzi wako. Kubaki bila kuoa au kuolewa haileti upungufu wowote kwa ubinadamu wako.
Lakini kama bado uko peke yako na una shauku kuoa au kuolewa, usitafute tu mtu yeyote. Bali tulia na umtegemee Mungu kwamba atakuletea yule ambaye atakufaa ukae naye. Subiri yule ambaye YEYE mwenyewe amekuchagulia. Kwa sababu kwako kilicho bora ni kubaki bila kuoa au kuolewa kuliko kufunga ndoa na mtu asiyefaaa, si kweli?!
Halafu sisi ambao tayari tumeshafunga ndoa … jamani tuache kabisa kuhukumu wale ambao hawajafunga ndoa. Mashujaa maarufu kabisa wa imani katika historia walikuwa wanaume ambao hawakuoa na wanawake pia ambao hawakuolewa.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.