Kukataa Kuwa Mtu wa Kawaida
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.
Yohana 1:12,13 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
Ni hatua kubwa – kubwa mno – kumwamini Yesu. kwamba alikuja kukuokoa na kukupa maisha mapya.
Na kama ulishachukua hatua ile, ujue kwamba kimetokea kitu kisicho cha kawaida, kitu ambacho kingekuwa rahisi kutokuelewa katika pirika za maisha ya kila siku. Kisikiliza:
Yohana 1:12,13 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
Ndiyo maana Yesu alisema, “Lazima mtu azaliwe tena ili aweze kuingia katika Ufalme wa Mungu.”
Wakati mtu anampokea Yesu kwa kumwamini na kutegemea kazi yake aliyomfanyia pale msalabani kwa kuchukua hatia ya makosa aliyoyafanya ili asamehewe na Mungu … ndipo atakuwa amezaliwa tena. Si kwa tafsiri ya kibinadamu, bali na Mungu mwenyewe!
Ebu fikiria kidogo. Umekuwa sasa mtoto wa Mungu aliye hai. Kujua hayo yangefanya uache kuishi maisha ya kawaida. Muda umewadia, kwa kweli, kukumbuka wewe ni mwana au binti wa nani na kukataa kuishi maisha ya kawaida. Kwa sababu Mungu amekusudia kutenda makuu ndani yako.
Punde tu ulipomwamini Yesu, alikupa kibali cha kufanyika mtoto wake.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.