... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Maisha Hayakukusudiwa Kuwa Rahisi

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 4:1,2 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.

Listen to the radio broadcast of

Maisha Hayakukusudiwa Kuwa Rahisi


Download audio file

Majaribu huwa yana tabia yakukunyemelea bila wewe kujua.  Ghafla unajikuta umeangushwa ndani ya dhambi huku ukijiuliza, Hayo yametoka wapi?

Kama hayo yamekutokea mara kwa mara, basi nikwambie kwamba hauko peke yako!  Huwa yanatutokea sisi sote.  Kwasababu majaribu hayawezi kulegea. Yaani yanazidi kuendelea … adui, ambaye ni Ibilisi haachi kukusumbua.  Hayo yalimtokea hata Yesu.

Mathayo 4:1,2  Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.  Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.

Mara tu baada ya ubatizo, Roho Mtakatifu alimshukia katika umbo la njiwa, mbingu zikafunguka na Mungu akatamka, “Huyu ndiye Mwanangu mpendwa wangu, ninayependezwa naye,”… punde tu  Yesu aliongozwa nyikani, Roho akamtoa kabisa na kumtupa huko, afunge siku arobaini, mchana na usiku halafu akiwa amelegea sana, ndipo alijaribiwa na Shetani.

Kwa kuwa imemtokea Yesu, kwanini tunafikiri kwamba sisi hatuwezi kujaribiwa, wewe na mimi?  Kwanini kushangaa kila wakati jaribu baya linapotuinukia? 

Hakuna siku hata moja ambayo hutajaribiwa ili utende dhambi. dhambi iko kazini daima, ikijaribu mtu na kumshawishi, ikitaka kupandikiza uovu maishani mwetu, tusishangae

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy