... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Msingi wa Uwezeshaji

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Matendo 1:8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Listen to the radio broadcast of

Msingi wa Uwezeshaji


Download audio file

Najua tunafahamuu vizuri kama tuna mapungufu; kwamba inatubidi turekebishe hapa na pale katika maisha yetu.  Lakini ni vigumu mno kujilinda kotekote.

Yesu anataka tumtii.  Anatuagiza tupende wasiopendeza, na kuwa vielelezo.  Yaani madai yake ni kama hayana mwisho.  Kwahiyo, mtu hata kama ameshachoka, bado atajihukumu hasa pale atakaposhindwa kukidhi vigezo.

 Kwa kweli, kubanwa kule ili mtu afaulu katika sekta zote; kunasumbua kabisa.  kunachosha.  Laiti ningekuwa mtu bora.  Laiti ningefanana zaidi na Yesu kuliko nilivyo.  Lakini, Ni lini ulifikia maamuzi kwamba yote lazima yatoke kwako; kwamba unapaswa kufaulu peke yako?

Wanafunzi wa Yesu walikuwa dhaifu, wenye hofu.  Walishuhudia alivyotendewa jeuri na kusulibiwa na hatimaye kufufuliwa kimiujiza. Hao ndio aliweza kuwaambia maneno yafuatayo:

Matendo 1:8  Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

Sasa uwezo huo wa Roho Mtakatifu ni kwaajili ya wewe na mimi, na kwa kila mtu anayemwamini Yesu.  Ni nguvu ya kuwa mtakatifu.  Nguvu ya kuwa mtu aliyekusudia uwe wakati anakuumba.  Nguvu ya kutenda mema, kupenda na kumulika nuru yake kwenye ulimwengu huu uliopotea na kuumia.

Hakuna sababu ya kutumika peke yako.  Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.