... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Ni Kipi Kitakachopindua Maisha Yako?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 4:12,13,17 Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kaperenaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali ... Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

Listen to the radio broadcast of

Ni Kipi Kitakachopindua Maisha Yako?


Download audio file

Ulimwenguni na hata kwa watu wa Mungu, kuna ujinga mkubwa kumhusu Yesu kwa kile Biblia inachokisema kuwa yeye ni nani, alifundisha nini, na alifanya nini.

Kama hutaki kusumbuliwa ili uendelee na maisha yako ya starehe bila kuwa na changamoto wala madai ni bora uendelee kuishi kwenye ujinga wa kutofahamu asili Yesu.  Sitanii.  Maisha ya starehe yanaendana na kubuni fikra zako kumhusu Yesu.

Niamini kabisa, nikisema kwamba siku moja mambo yatakuharibikia.  Itafika mahala uovu wa ulimwengu huu au dhambi zako zenyewe au vyote viwili vitaungana pamoja  na kupindua vibaya maisha yako.

Mathayo 4:12,13,17  Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya; akatoka Nazareti, akaja akakaa Kaperenaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali …  Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

Bila shaka, swala zima la “toba”, yaani kuachana na mambo unayoyajua kuwa  ni mabaya, kuacha sehemu yako ya anasa na starehe wakati mambo yanaenda kombo… yote yatasababisha maisha yako yapinduliwe.  Maisha hayawezi tena kuendelea kama ulivyopanga.

Bora kumwachia Yesu arekebisha dira yako ili uelekezwe vizuri kuliko kuacha uovu wako ukuangamize.

Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy