... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Habari Njema na Habari Mbaya

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Matendo 17:30,31 Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu. Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.

Listen to the radio broadcast of

Habari Njema na Habari Mbaya


Download audio file

Leo kuna habari njema na habari mbaya.  Tuanze na Habari Njema: Mungu anakupenda kuliko ninavyoweza kueleza na Yesu alikuja kwa kusudi la kufa kwa ajili ya dhambi zako ili uweze kusamehewa kabisa.  Habari mbaya ni kwamba, hatimaye kama unaamua kutokupokea habari njema hiyo na kuiishia, basi Mungu atakuhukumu na kukutupa Jehanamu, kuishi mbali na Kristo milele daima.

Najua, kwamba katika karne hii yetu ya 21 wengi wanafikiri kwamba habari hizo ni za upuuzi tu.  Je!  Kwa kweli Wakristo wale bado wanatuletea takataka hizo?  Inawezekanaje Mungu wao wa upendo kutupa watu Jehanamu?  Jamani!  Au labda wewe mwenyewe moyoni mwako unaamini Habari Njema ya Yesu, lakini mwenendo wako unakusuta na kukukosesha amani.  Po pote ulipo, sikiliza basi maoni ya Mungu mwenyewe kuhusu mada hii:

Matendo 17:30,31  Basi, zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hazioni; bali sasa anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu.  Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu.

Ni kweli, lazima tuamini na kuweka tumaini letu kwake Yesu.  Lakini sehemu muhimu ya Habari hii Njema ni mwitikio wetu – yaani kubadilika na kumgeukia.  Kama vile A.W. Tozer alivyoeleza, “Dhana kwamba Mungu angemsamehe muasi ambaye hajaacha uasi wake ni kinyume kabisa na Maandiko hata maarifa ya kawaida.”

Badilika na kumgeukia.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.