... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Jinsi Unavyokuwa Mkarimu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luke 6:38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

Listen to the radio broadcast of

Jinsi Unavyokuwa Mkarimu


Download audio file

Je!  Utakwazika nikikuuliza swali hili?  Je!  Wewe ni mkarimu kiasi gani kwa kusaidia watu wengine?  Wakati unamwona mhitaji, mara moja mwitikio wako ukoje?

Ukarimu uko kwingi.  Mtu anaweza kuwa mkarimu kwa kushukuru, kwa wema, kwa kuelewa watu, kwa kutumia muda wake na ni dhairi anaweza kuonyesha ukarimu kwa kutoa katika rasilimali aliyo nayo.

Ni rahisi sana tukiwa bize katika pirika za maisha, wakati sisi wenyewe tumebanwa na tukiwa na hamu ya kufadhiliwa na kusaidiwa, ni rahisi kuanza kuwa na mtazamo wa bahili.  Sasa tukiendelea na mtazamo huo, tutazidi kushuka na kuona baraka tulizodhani tulikuwa nazo zinatoweka.

Kama umejikuta katika hali kama hiyo, au kama baada ya kutafakari kidogo unaweza kukiri kwamba umekuwa bahili kiasi fulani, acha maneno ya Yesu yawe kama tiba kwa ajili ya nafsi yako:

Luke 6:38  Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu.  Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

Sina uhakika kwamba maneno hayo tunaweza kuyashika kama ahadi lakini nadhani yanaeleza hali halisi ya mambo.  Ndivyo mambo yanavyoenda.  Ni yupi katika wale ambao unaoweza kuwashawishi anahitaji kuguswa na ukarimu wako leo hii?  Neno la kumtia moyo, kumtendea mema na ikiwezekana kumsaidia kwa kumtolea kitu katika mali uliyo nayo?

Jinsi unavyowagawia watu wengine, ndivyo Mungu atakugawia.  Uwe mkarimu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.