... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Imani Ishindayo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Yohana 5:3-5 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito. Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?

Listen to the radio broadcast of

Imani Ishindayo

Download audio file

Kwa nini Mungu anaruhusu tupitie mateso na maumivu?  Kwa nini unapaswa kukabiliana na matatizo yaliyo mbele yako sasa hivi?  Je!  Kwa nini mambo yasiwe rahisi kwa wale wanaomwamini Yesu?

Matajiri, maskini, walioonewa na walio huru, wakati wa vita, wakati wa amani utapata mateso mara kwa mara.  Kupata mateso ni sehemu ya maisha ya kila mwanadamu.  Hayaepukiki.

Mungu, kwa nini umeruhusu?

Ningekupa jibu la kiteolojia kwa swali hilo – kwamba dhambi ya binadamu kuanzia Adamu na Hawa na tunda lile haramu, ni mzizi  wa matatizo yote.  Lakini labda yafuatayo yatakusaidia:

1 Yohana 5:3-5  Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.  Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.  Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?

Ushindi mtamu unaoshinda yote maishani mwako … ni imani yako kama kweli inazidi kuimarika.

Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu?  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.