... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Inatosha!

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 4:29 Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

Listen to the radio broadcast of

Inatosha!


Download audio file

Siku hizi ukosoaji na ugomvi ni kama umekuwa mfumo wa kawaida katika mahusiano.  Likiwa swala la siasa, maoni, jamii na hata la imani, ni kama kila mtu anataka kuwakosoa watu wengine.

Si katika mawasiliano ya umma tu, lakini hata mawasiliano kati ya watu na watu.  Siku hizi kila mtu amepewa sauti kupitia mtandao, kwa hiyo wakosoaji wamezidi kabisa.

Acha nikuulize ili tuweze kujipima.  Je!  Umeshiriki kiasi gani kwa kukosoa na kubomoa watu wengine katika masaha 24 yaliyopita?  Labda si kumkosoa mtu ana kwa ana, lakini kukosoa kimya kimya watu unaofanya kazi nao, labda mtu wa familia yako au viongozi wanaotawala nchi yako?  Mtu akijikagua hivyo, kumbe!  Inatisha kweli!

Kwa hiyo, ukitafakari maswali hayo, tuwe tunachunguza anachokisema Mungu kuhusu ukosoaji uliopo duniani mwetu:

Waefeso 4:29  Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia.

Ebu fikiria ingekuwaji kama wewe na mimi, tungeamua tofauti kabisa katika mazingira ya ukosoaji; kama tungeamua kuongea kwa upole, kuwatia moyo wengine badala ya kuwakosoa; kuwajenga na kuwabariki kupitia maneno yetu.  Je!  Ulimwengu wetu ungebadilikaje, kama tungefanay hivyo?

Katika ulimwenguni uliojaa wakosoaji, wewe unaweza kuchagua kuwa mtu anayetia moyo watu wengine.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.