... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kukaa Bila Kuoa au Kuolewa (2)

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 7:32-35 Lakini nataka msiwe na masumbufu. Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje; bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atavyompendeza mkewe. Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe. Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine.

Listen to the radio broadcast of

Kukaa Bila Kuoa au Kuolewa (2)

Download audio file

Leo ninataka kukushirikisha jambo la maana sana kuhusu wao wanaoendelea kukaa bila kuoa au kuolewa.  Labda wewe si mmojawapo lakini bila shaka unafahamiana na mtu wa namna hiyo. Kama unamjua, basi jaribu kumshirikisha na yeye ujumbe huu.

Hata tusipotaka kukubali, sisi ambao tumeshafunga ndoa tuna tabia ya kudharau wale ambao hawajaoa na kuolewa. Hivi umewahi kujiuliza habari ya mtu fulani, “Kwanini hajaoa au hajaolewa, na ana tatizo gani? 

Huko Japan kwa mfano, jina lenye dharau wanalolitumia kwa mwanamke ambaye hajaolewa ni “keki ya Krismasi iliyochina.”  Lakini si kwamba tunavizia watu wa Japan.  Mtazamo huo upo kwenye tamaduni karibuni kote duniani huwa tunjiuliza juu ya watu wazima ambao hawajaoa kuwa wanatatizo gani.  Lakini mtazamo huo ninataka tuufute kabisa mioyoni mwetu:

1 Wakorintho 7:32-35  Lakini nataka msiwe na masumbufu.  Yeye asiyeoa hujishughulisha na mambo ya Bwana, ampendezeje; bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atavyompendeza mkewe.  Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali.  Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho.  Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.  Nasema hayo niwafaidie, si kwamba niwategee tanzi, bali kwa ajili ya vile vipendezavyo, tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine. 

Usiwadharau wale ambao hawajafunga ndoa.  wito wao ni wa hali ya juu zaidi! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.