... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Muda Mwafaka wa Utendaji

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yoshua 1:10,11 Ndipo Yoshua akawaamuru maakida wa watu, akisema, Piteni katikati ya matuo, mkawaamuru hao watu, mkisema, Fanyeni tayari vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, mpate kuimiliki.

Listen to the radio broadcast of

Muda Mwafaka wa Utendaji

Download audio file

Wakati safari yetu inatuwia vigumu, hisia za hofu na fadhaa, hua zinatulemaza.  Ni kama mnyama anayeshitukizwa barabarani akijikuta ndani ya mwangaza wa taa za gari usiku, ndivyo nasi tunashindwa kufanya lo lote, hasa yale yanayotakiwa yafanyiwe wakati ule ule.

Jana tulimkuta Yoshua kipindi kinachotisha.  Musa alikuwa ameshakufa.  Yoshua amekuwa sasa kiongozi wa Israeli kipindi iliwalazimu kuanza mapigano endelevu kwa kuishika Nchi ya Ahadi.  .    

Sasa mwitikio wa Yoshua ulikuwaje?  Nguvu na ujasiri vilivyotoka kwa Mungu vilidhihirikaje?

Yoshua 1:10,11  Ndipo Yoshua akawaamuru maakida wa watu, akisema, Piteni katikati ya matuo, mkawaamuru hao watu, mkisema, Fanyeni tayari vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu, mpate kuimiliki.

Nguvu na ujasiri Mungu alimkirimia Yoshua, vilidhihirika kiutendaji.  Badala ya kubaki huku upande salama wa Yorodani, alikuwa hodari kwa kuiandaa taifa kwa ajili ya vita, kuvuka mto na kushika Nchi ya Ahadi.

Usiruhusu hofu na fadhaa zikulemaze.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.