... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tazamo Lako la Mara Moja

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Ufunuo 7:9,10 Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.

Listen to the radio broadcast of

Tazamo Lako la Mara Moja

Download audio file

Je!  Umewahi kutaka kutazama angalau mara moja kwenye umilele?  Itakuaje?  Je!  Mapambano tunayo leo, yatafidiwa kweli kweli tukiishi milele na Mungu huko ng’ambo?

Mimi ninahisi kwamba mtu awaye yote aliyekusudia kumwishia Yesu amewahi kujiuliza mara kwa mara, Je!  Ina maana yo yote masumbuko hayo yote?

Ni swali linalofaa kabisa.  Kuna siku tunajaribiwa kuachilia na kwenda na mkondo wa dunia hii, kula, kunywa na kufurahi tu.  Kukubali kutawaliwa na hila, kiburi, na ufisadi vya ulimwengu huu ambavyo vimekuwa kawaida siku hizi.

Kwa kukusaidia kujibu swali lako wewe mwenyewe, leo hii ninakupa tazamo la mara moja kwenye umilele:

Ufunuo 7:9,10  Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo.

Kama unamwamini Yesu, siku moja, ukiendelea kuwa mwaminifu kwake, utasimama ndani ya umati ule wa watu … na utamwabudu milele daima.  Kwa kweli ina maana kabisa, inafaa!  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.