... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Usiache Kuomba

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 18:6,7 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu. Na Mungu je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?

Listen to the radio broadcast of

Usiache Kuomba


Download audio file

Je!  Umewahi kujisikia kwamba hupati majibu unayohitaji; kwamba unanyimwa mafanikio mapya; kwamba Mungu hakusikilizi au hajali?  Basi leo hii, Yesu ana somo kwa ajili yako kama umejikuta katika hali kama hiyo.

Yesu alifundisha wanafunzi wake kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.  Alitumia mfano ufuatao ili akazie mada yake.

Palikuwa na hakimu ambaye hamchi Mungu, wala hajali watu.  Sasa kulikuwa mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu!  Lakini hakimu alimkatalia.

Kwa hiyo yule mama aliendelea kumsumbua-sumbua, hadi alisema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.

Kwa kweli ni njia inayoshangaza kutumia kwa kufundisha wanafunzi wake kuhusu tumaini.  Kumbe anatoa mfano wa mtu mbaya kuwatia moyo wanafunzi wake!

Luka 18:6,7  Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.  Na Mungu je!  Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?

Kitu ambacho Yesu anataka kutufundisha hapa ni kwamba hata kama mazingira yako kinyume nasi, bado tunapaswa kushikilia kabisa dua letu.

Endelea kuomba, usikatishwe tamaa.  Mungu atakupa haki. Hatakawia kukusaidia!

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.